
Mkopo huu umebuniwa kwa watu binafsi na makampuni yanayotaka kununua magari ya kibiashara kama vile malori, mabasi na matipa. Tunakulipia hadi 60% ya thamani ya gari, iwe jipya au lililotumika kutoka nje ya nchi, hivyo kukusaidia kukuza biashara yako.
Marejesho ni hadi miezi 24, kwa masharti nafuu na rahisi yanayokuwezesha kufanikisha malengo ya biashara yako ya muda mrefu. Iwe ni kwa mizigo, usambazaji au kuongeza idadi ya magari – tuko hapa kuhakikisha unafanikiwa.
i. Vigezo vya kupata mkopo
- Raia wa Tanzania kati ya umri wa miaka 18 hadi 65.
- Wafanyakazi waliothibitishwa wa taasisi za umma na binafsi.
- Wajasiriamali binafsi na wataalamu.
- Wafanyabiashara na makampuni.
ii. Sifa za Mkopo
- Mkopo hadi 60% ya thamani ya gari.
- Marejesho hadi miezi 24.
- Riba za ushindani.
- Pata funguo zako ndani ya saa 72 baada ya kuwasilisha nyaraka.
- Mkopo hadi TZS 100,000,000.
Apply Your Loan Now
Determine your repayment plan using this simple loan calculator.
Selected: 3 months