
Jumanne, 8 Machi 2022
Uwekezaji huu mkubwa mpya umefungua njia kwa kampuni kuharakisha malengo yake ya ukuaji na kuendelea kuwasaidia wateja wake.
Mwaka wa 2021 uliiona Tujijenge Tanzania Financial Services Ltd ikipokea msukumo mkubwa wa kimkakati wa kifedha na uaminifu kwa njia ya uwekezaji wa kimkakati wa Shilingi bilioni 6 kutoka LOLC Mauritius Holdings Limited. Kupitia uwekezaji huu, Tujijenge Tanzania imeimarisha mtaji wake, jambo lililowezesha kuendeleza mipango yake ya ukuaji wa kibiashara na kutimiza kikamilifu mahitaji yake ya uendeshaji.
Kuhusu LOLC
LOLC inachukuliwa sana kama kundi la kifedha lenye thamani kubwa zaidi kutoka Sri Lanka lenye uwekezaji tofauti duniani, na imeshikilia nafasi ya juu kama shirika linalopata faida kubwa zaidi lililoorodheshwa katika Toleo la 28 la LMD Top 100 kwa mwaka wa 2020/21. Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa LOLC kushikilia nafasi hiyo ya kwanza.
LOLC inatambuliwa kama shirika lenye faida kubwa zaidi nchini Sri Lanka, taasisi kubwa zaidi ya kifedha isiyo ya kibenki, na mojawapo ya makampuni yenye uwekezaji wa kimkakati tofauti. Kundi la LOLC linajishughulisha kimataifa na sekta za burudani, mashamba, kilimo, nishati mbadala, ujenzi na mali isiyohamishika, uzalishaji na biashara, teknolojia, utafiti na ubunifu pamoja na sekta nyingine muhimu za biashara. Kama kiongozi katika sekta ya MSME nchini Sri Lanka, Kundi la LOLC limekuwa chachu ya kuendeleza ujumuishwaji wa kifedha, huku likijitahidi kuongeza manufaa kwa mazingira kupitia shughuli na michakato ya kijani kulingana na mwelekeo wake wa kijamii, kiuchumi na kimazingira (triple bottom line).
Baada ya miaka kadhaa kama shirika kuu kwenye soko la ndani, Kundi la LOLC sasa linafanya hatua kubwa katika masoko ya kimataifa pia. Kwa malengo ya kurudia mafanikio yake ya ndani katika ngazi ya kimataifa, Kundi la LOLC tayari limejijengea sifa kama kiongozi wa kimataifa katika jukwaa la mikopo midogo lenye fedha nyingi na maeneo mengi, likiendesha Taasisi za Kifedha Zisizo za Kibenki katika nchi nane. Mafanikio haya yameongezewa nguvu na mifumo ya teknolojia ya hali ya juu iliyobuniwa na shughuli zake za Sri Lanka na sasa inatumiwa pia na kampuni zake za kimataifa.
Kwa maelezo zaidi kuhusu LOLC, tembelea tovuti yao www.lolc.co.tz.