
Tunapenda kuwajulisha kuwa, kwa idhini ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), jina la kampuni yetu limebadilishwa rasmi.
Awali kampuni yetu ilijulikana kama Tujijenge Tanzania Financial Services Limited, na kuanzia tarehe 1 Novemba 2024, itajulikana kama LOLC Tanzania Financial Services Limited.
Tafadhali fahamu kuwa, isipokuwa mabadiliko ya jina, hakuna mabadiliko mengine katika shughuli zetu za biashara, bidhaa, au huduma tunazotoa. Tunaendelea kujitolea kukuhudumia kwa uaminifu na ubora uleule.
Kwa maswali au ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
📧 Barua pepe: lolctanzania@lolc.co.tz
📱 Simu: +255 739 611 612 / +255 736 611 617